You are here:  / Campaigns in Bomet / Campaigns In Kajiado / Joho's speech / Jubilee Manifesto / NASA manifesto / Political Review / Politics / “Uhuru ni mlevi na Ruto ni Mwizi”; Joho Speech In Bomet. 

“Uhuru ni mlevi na Ruto ni Mwizi”; Joho Speech In Bomet. 

Spread the love

According to Joho; does it mean that our country is being governed by thief and drunkard persons? (Ruto and Uhuru respectively)

Bomet hoyee… Bomet mamboo… Mko gangari? Mko gangari kinoma? Mko tayari? Basi mimi ndiyo Yule Yule jamaa kutoka Mombasa. Mimi ndiyo yule yule Uhuru Kenyatta wananifungia njia! Ilekitu amesahau kunifungia ni mdomo wangu na nikonayo hapa Bomet leo.  Sa nimekuja hapa niwaambie namna hii; ilemara ingine tulikuwa hapa tukiongea namna hii, tuliona vijana wengine kulee wakifanya maajabu. Lakini mimi leo naenda kuwaambia watu wa Mombasa, nimekuwa Bomet na nimeona rift ime shift.

Nimekuwa Bomet na nimeona rift ime shift, Nami nataka kuanzia pale my brother Isaac amewachia. Niseme namna hii; Uhuru Kenyatta amezoea kusema uongo na kwasababu hao ni waongo, Minataka kuchukua hii njia Isaac Ruto amauchukuwa. Kama ni ukweli mnataka kufanya elimu iwebure? Na nyinyi Mko serikalini. Mna mabilioni ya pesa ikokatika serikali yenu, tuma mpesa kwa watu ambao wamelipa school fees Januari kuanzia leo.

Nakama hutumi mpesa, hauna haja yakuongea mambo ya school fees kwasababu ni uongo wa kawaida huo.

Unajuwa wacha niwaambie mfano wa Jubilee; Umewai kuenda bus stop? Ukifika bus stop, uonebasi imebaki bure. Ukiona derevaa… Ni Mlevi, ukiangalia vizuri unaona conductor ni Mwizi. Dereva mlevi… Conductor Mwizi! Hiyo ndiyo Jubilee hiyo. Hiyo ndiyo nini?  Jubilee. Ndio mana nimekuja hapa mimi mwenyewe, kuona yakwamba hii rift ina shift kwasababu ni muhimu sana kwetu.

Nami nataka niwaambie namna hii, kunatofauti ya ule Ruto mwingine na huyu Ruto huyu wetu. Tofauti moja muhimu watu wabomet mnafaa mjue ni kwamba Ruto huyu mzuri, hakona future mzuri. Tunaelewana? Hajaiba Mali ya mtu, hajapeana watu kipindupindu, hajachukua shamba ya mtu, hakuna namna anaweza kuishia mahali pabaya. Si namna hiyo; Ule Ruto mwingine… Mimi nimebadilisha jina yake: Sisi waswahili tunasemanga, Mwizi ni Mwizi hakuna njia ningine.

Nami nataka niwaambie nyinyi wakenya wenzangu, ukienda nyumbani leo; Chukua karatasi na kalamu andika tu hesabu and i am serious. Kwasababu hii mimi ni kijana my friend, what happens in 2017 election ina affect maisha yangu ya siku ya usoni. So hii kwetu ni very very serious business, si namna hiyo?  Tunataka tuone maisha yetu ikinyorosheka na maisha ya watoto wetu. Nami nataka huende ukachukue kalamu na karatasi leo Joni. Uandike pale bei ya Unga, bei ya transport, bei ya maziwa, bei ya Sukari, bei ya kodi ya nyumba yakulipa, bei yashule ya kulipa na uweke hiyo. Miaka sita iliyopita wakati Kalonzo  Musyoka alikuwa vice president, Raila Odinga alikuwa Prime Minister na Kibaki alikuwa president na compare that na hii ya Uhuru na Ruto mwaka huu, 2017.

Tena unajua mimi nashangaa bana, out of 45 million Kenyans, Out of 45 million Kenyans you cannot have William Ruto talking about corruption. Wakenya million arubaini na nne, hello, someone like Stephen Kalonzo Musyoka akiongea mambo ya ufisadi; wakenya wanafaa wamskie sababu amajulikana kuwa msafi Kama bamba. Hakuna siku ambao ufisadi umemlegea hata siku moja.

My father, my leader and my party leader Raila Odinga amepigana na ufisadi katika mwaka hii mpaka amaokoa Kenya mnajua mambo ya NYS, eurobond na zingineo. Unajua mimi nataka niwaambie ile SGR, unfortunately walejamaa wameifanya iwe very expensive. Na Unajua mimi nimewaambia watu wa riftvalley, mnasemanga William Ruto ni wenu? Kama ni wenu angehakikisha hiyo SGR, imekuja Eldoret na hapa Bomewe

Kwani wewe unaejoyiwa enjoyiwa ati yeye ni wetu, mbona SGR imeenda Naivasha kwanza? Na ukulima woote mkowapi? Bonde la ufa si namna hiyo. Ndiyo tumeambia hawa na serikali ya Raila Odinga na Kalonzo Musyoka ikiingia tutatoka hii inchi wameanza kuzoga katika mambo ya kuimport Mali Kenya. We want to shift that so that we create a balance, Mali yakuwa exported na Mali yakuwa imported. Hataukiangalia maesabu yao na hapa malipo ya mikopo yao wanaiweka kwanjia ya kwamba watalipa madeni kwa mali wataileta kutoka China.

Sinamna hiyo? Nami nataka niwakumbushe, mkienda bus stop , mkienda nini bus stop. Uonebasi liko hapo, dereva ni mlevi na conductor ni nini? Mwizi. Msiwahi panda hiyo Basi na hiyo ni Jubilee, Asanteni.

Comments From Facebook

Sir Daniel Omondi Is an Entrepreneur | Web/Blog Designer | Passionate Blogger in Personal Development, Politics and Entertainment | Passionate Deejay. Am competing with my best abilities; So should you. In determining your talent(s) you have to have a vast variety of abilities.

%d bloggers like this:
Skip to toolbar